Press ? for keyboard shortcuts.
Mfadhili
wa fainali za kombe la Ng"ombe jijini Arusha,Kim Fute akimkabidhi
zawadi ya ng"ombe kocha wa klabu ya Zamzam,Omary Athuman mara baada ya
timu yake kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0 jana katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Wachezaji wakiwa wanapambana uwanjani
Mfadhili
wa fainali za kombe la Ng"ombe jijini Arusha,Kim Fute akimkabidhi
zawadi ya Jezi kocha wa klabu ya Zamzam,Omary Athuman mara baada ya timu
yake kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0 jana katika uwanja
wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha
Mashabiki wakiwa wa timu ya Zamzam wakiwa wanashuhudia zawadi ya ng'ombe baada ya timu yao kushinda kwa mabao 2-0
Mfadhili wa fainali za kombe la Ng"ombe jijini Arusha,Kim Fute akiwa anazungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi
Umati mkubwa wa mashabiki wa timu ya Zamzam na Nyota wakifatilia mpambano
Mashabiki
mbalimbali wakiwa katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha
wakishuhudia mchezo wa fainali baina ya Nyota na Zamzam zilizokutana
katika uwanja huo jana,Zamzam waliibuka mabingwa baada ya kuilaza Nyota kwa mabao 2-0
Mratibu
wa mashindano hayo Sanare Mollel akizungumza na wanahabari kuhusu mechi
hiyo iliyokuwa ikifanyika katika uwanja wa shule ya Sinoni jijini
Arusha
Taswira katika uwanja huo wa shule ya Sinoni jijini Arusha
Mashabiki
wa klabu ya Zamzam wakimyanyua mlinda mlango wa klabu hiyo mara baada
ya timu yake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa fainali ya kombe la Ng"ombe
baada ya kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0 juzi katika
uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha
Kushoto
ni mdau mkubwa wa mtandao wa kijamii wa Jamiiblog Muhamed Akonaay
akiwa na mmiliki wa mtandao huo Pamela Mollel katika uwanja wa sinoni
Klabu
ya Zamzam yenye maskani yake Sinoni jijini Arusha juzi wamefanikiwa
kutwaa ubingwa wa kombe la Ng”ombe mara baada ya kuilaza klabu ya Nyota
kwa jumla ya mabao 2-0.
Kwa
ushindi huo Zamzam walikabidhiwa zawadi ya ng”ombe na jezi huku Nyota
wakiambulia zawadi ya seti moja ya jezi kama mshindi wa pili katika
fainali iliyopigwa katika uwanja wa shule ya msingi ya Sinoni jijini
Arusha.
Katika
mchezo huo wa fainali ambao ulikuwa na mbwebwe za kila aina kipindi cha
kwanza kilimalizika bila timu yoyote kuona lango la mwenzake huku
mlinda mlango wa Zamzam,Seleman Msuya maarufu kama “Casillas”akionekana
kung”ara katika mchezo huo.
Kipindi cha pili kilipowadia klabu ya Zamzam ilifanikiwa kupata mabao kupitia kwa wachezaji wake Jaff Mbunda dakika ya 50 na Juma Mgunya dakika ya 82 na kupelekea shangwe kwa klabu hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi zawadi hizo,mfadhili wa ligi hiyo,Kim Fute
ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya East Link Tz Ltd alisema kuwa
lengo kuu la kudhamini fainali hizo ni kuibua vipaji na kusisitiza pia
michezo inaondoa tofauti za kidini,kisiasa,kikabila na kuleta umoja.
Naye,mratibu
wa michuano hiyo,Richard Mollel alisema kuwa jumla ya timu 12 katika
kata mbalimbali za halmashauri ya jiji la Arusha huku lengo lake likiwa
ni kuibua vipaji na kuleta umoja ndani ya jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni