Jumanne, 19 Mei 2015

SERIKALI YARIDHISHWA NA MADINI YALIONDALIWA

SERIKALI imesema kuwa imeridhishwa na maonyesho ya madini ya vito yaliyoandaliwa na  jumuia ya wafanyabiashara wa madini nchini Tamida,kutokana na kuonyesha mafanikio makubwa  yakiongozwa na madini ya Tanzanite.

Waziri wa Nishati  na Madini,Georage  Simba Chawaene,ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua maonyesho ya nne ya madini ya vito yanayoshirikisha wauzaji, wanunuzi wakubwa wa madini hayo ulimwenguni .

Chawene,amesema kuwa hivi sasa serikali ipo katika hatua za uimarishaji wa kutengenezaji madini  ukataji wake na uchongaji  hivyo kuyauza yakiwa yameongezewa thamani na kutoa ajira  nyingi tofauti na awali ambapo yalikuwa hayatoi ajira hizo kutokana na kuuzwa yakiwa ghafi.

Amongeza kuwa serikali ipo katika hatua za mwisho kutengeneza kituo kikubwa cha kuuzia madini ambapo kutakuwepo na Hotel, maduka na ofisi za mamlaka ya mapato TRA, na uwanja wa kutua Helkopta  na hivyo kuondoa ulanguzi wa madinin na hivyo kuongeza pato la taifa sanjari na kuondoa urasimu uliokuwepo wakati wa mauzo ya madini.

Pia serikali itaweka  vituo maalumu vya ukaguzi  kwenye machimbo ya Tanzanite,ili kudhibiti wizi sanjari  na kurejesha  utaratibu wa kujenga ukuta uliokuwepo kwenye machimbo hayo  ambao ulibomolewa na baadhi ya watu wenye nia mbaya ili waweze kutorosha madini hayo kwa urahisi ,pia kuimarisha  ,utolewaji wa vitambulisho .
 
Ameongeza kuwa utoroshaji wa madini unaofanywa na watanzania ambao wamepewa leseni za kuuza na kununua madini umepungua kutokana na udhibiti kuimarishwa.

Amesem,a miaka miwili iliyopita Tanzania ilipata dola milioni 38 za kimarekani kutokana na mauzo ya Tanzanite, huku Kenya ikipata dola milioni 100 kutokana na mauzo ya Tanzanite, na India ilipata dola milioni 300.
 
 
 
Arusha.
RAIS Jakaya Kikwete, anatarajiwa kumtunuku tuzo maalumu ,Jumaine Ngoma,ambae ni mgunduzi wa madini ya Tanzanite.
Waziri wa Nishati na madini, George Simba Chawene, ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonyesho ya nne ya madini ya vito .

Amesema kuwa rais, atatoa tuzo hiyo kutokana na kuthamini mchango wa Mtanzania huyo ambae aligundua madini hayo ambayo yanathamani kubwa ulimwenguni.

Madini ya Tanzanite , ulimwenguni yanapatika kwenye machimbo ya madini ya Mirerani ,wilayani simanjiro mkoani Manyara.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni