Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha,Ferooz Bano wakati akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho,Kim Fute
Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani hapa kujitambulisha na kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.
Hadi sasa jumla ya wagombea saba ambao ni Kim Fute,Phillemon Mollel”Monaban”,Mustapha Panju”Bushbuck”,Victor Njau,David Rwenyagira,Deo Mtui,Francis Laiser pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini,Felix Mrema wamejitokeza kutia nia kuwania jimbo la Arusha mjini.
Akizungumza mara baada kumkabidhi kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutiania kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa wapiga kura.
“Muda wa kampeni bado haujafika hatutaki nyinyi wagombea muanzekuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano
Hatahivyo,kwa upande wake mgombea huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya chama hicho na kusisitiz kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini mkubwa.
Fute,alitangaza rasmi kuinga katika kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe la uongozi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni