Ijumaa, 29 Mei 2015

WANAHABARI MKOA WA IRINGA NA POLISI WAKUTANA KATIKA KIKAO CHA MAHUSIANO MEMA

Baadhi ya wanahabari  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika picha  ya pamoja na viongozi  wa  jeshi la polisi mkoa wa Iringa mara baada ya  kumalizika  kikao  chao cha mahusiano mema na kutambulishana kati ya wanahabari na viongozi wapya wa  jeshi  la Polisi waliokaa ni kamanda wa polisi Ramadhan Mungi wa tatu  kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard na katibu wa IPC Francis Godwin na maofisa wengine wa polisi mkoa
Baadhi ya askari polisi wakiwa ktk kikao cha pamoja na wanahabari leo
Wanahabari Mkoa wa Iringa wakiwa ktk kikao cha pamoja na maofisa wa jeshi la Polisi




Wanahabari  wakiwa katika kikao na jeshi la polisi
Kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi akitoa mafunzo mafupi kwa  wanahabari kati ya utendaji kazi wa  jeshi la polisi na vyombo vya habari

 Na FG BLOG
Wanahabari wa mkoa wa Iringa leo wamekutana na kamanda wa polisi na maofisa wa jeshi la polisi Mkoani hapa ili kuendelea kufanya Kazi kwa ushirikiano kwa faida ya Mkoa wa Iringa.

Katika kikao hicho kilichoambatana na semina fupi ya kukumbushana wajibu wa Kazi za wanahabari na askari.

Akitoa mafunzo hayo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa ili kuufanya Mkoa wa Iringa uweze kufanikiwa ni lazima wabahabari na polisi kufanya Kazi zao kwa kuzingatia maadili na kutofanya upendeleo katika utendaji wao.

Mungi alisema kuwa mbali ya kazi kubwa ambazo vyombo vya habari mkoani hapa vinafanywa bado jeshi lake limeamua kukutana na wanahabari hao ili kizidi kuufanya Mkoa kuwa na taswira nzuri ktk mahusiano Kati ya pande hizo mbili kama njia ya kuwatumikia wananchi.

Alisema kwa Mkoa wa Iringa vyombo vya habari vimeonyesha mchango mkubwa zaidi zaidi na kutaka mchango huo na jitihada hizo kuendelea zaidi .

Kamanda Mungi amesema kuna haja ya wanahabari na askari polisi kuendelea kujenga mahusiano kwa kukutana na viongozi wao kabla ya kufanya mapambano yasiyo na tija.

Alisema kuwa wao kama jeshi la polisi wanatambua kuwa vyombo vya habari ni muhimu kwa jamii hivyo lazima kujenga mahusiano mema na kuwa askari polisi hawanasababu ya kuendeleza mivutano 

Alisema kuwa kuna wakati mwingine ajali imetokea na Kazi ya mwanahabari ni kuhabarisha umma na polisi kuokoa hivyo lazima kufanya Kazi kwa karibu na kutoa majibu stahiki kwa wanahabari na wanahabari kutotumia jazba katika utendaji Kazi zao 

Akizungumza katika mafunzo hayo  mwenyekiti wa chama cha  waandishi  wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard  alisema  kuwa hatua ya  jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuandaa kikao  hicho cha kufahamiana na mafunzo mafupi kwa wanahabari ni ya kupongezwa zaidi hasa kwa wakati  huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu .

Alisema  kuwa tofauti baina ya badhi ya askari na wanahabari  ilikuwa ikijitokeza kutokana na pande  hizo  mbili zinazofanya kazi za kijamii kutoatambuana vilivyo hivyo kila upande  kuonyesha chuki dhidi ya mwingine jambo ambalo halijengi bali hubomoa.

Leonard  alisema kikao  hicho  kina umuhimu mkubwa kwa wanahabari  hasa  wakati  huu  wa kuelekea  uchaguzi mkuu ambao baadhi ya askari  walikuwa  wakiwachukia wanahabari na  wanahabari  kuwachukia polisi hasa kutokana na matukio ya nyuma kabla ya Mungi  kuwa kamanda wa  polisi wa mkoa huo wa Iringa.

Katika  hatua  nyingine mwenyekiti  huyo aliomba  jeshi la polisi  kuwa  na utaratibu wa kukutana na  wanahabari japo kwa  mwezi mara moja  ili  kujitathimini  utendaji kazi wao na  pale  penye tofauti  basi  kuweza kuzimaliza kwa njia  sahihi kuliko kila mmoja kutumia nguvu zisizo na tija.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni