MFANYABIASHARA maarufu wa Madini ya Tanzanite mkazi wa jijini hapa,Eliakimu
Daud Mollel(45),amepandishwa kizimbani katika mahakama
ya hakimu mkazi Arusha akikabiliwa na shitaka la kujipatia madini ya thamani ya shilingi milioni 15 kwa njia ya udanganyifu.
Akisoma mashtaka mwishoni mwa wiki, mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Nestory Baro,mwendesha mashtaka wa serikali,Gaudencia Lyimo aliieleza mahakama hiyo kwamba, mshtakiwa alitenda kosa hilo januari 4 mwaka huu katika jengo la Ottu, huku akifahamu wazi kuwa ni
kinyume cha sheria .
Alisema mshtakiwa huyo alijipatia madini ya Tanzanite kutoka kwa mlalamikaji ,Banai Shininu yenye thamani ya shilingi milioni 15.

Ilidaiwa kuwa mfanyabiashara Mollel alimrubuni
mlalamikaji kuwa anaenda kuuza na baadae angemletea kiasi cha shilingi milioni 15,ikiwa
ni thamni ya madini hayo, hatua ambayo hakufanya hivyo badala yake alitoweka
kusikojulikana.
Mahakama
ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na mlalamikaji na
punde anapopatikana hutoa ahadi za uongo kuwa angelipa kiasi hicho cha fedha
lakini hakufanywa hivyo hadi alipokamatwa na kufikishwa mahakamani.
Baada ya
kusomewa shtaka hilo la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu,mshtakiwa alikana
kutenda kosa hilo .
Hata hivyo
hakimu Baro alimweleza mshtakiwa kwamba dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na fedha
tasilimu kiasi cha shilingi milioni 7.5,na
wadhamini wawili wanaofahamika hatua ambayo mshtakiwa alishindwa kutimiza na
kulazimika kwenda magereza.
Kesi hiyo namba 88 ya mwaka huu, imepangwa kutajwa
tena mahakamani hapo januari 26 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni