Jumatano, 20 Mei 2015

BALOZI SEIF ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya kukagua Nyumba zilizoathirika na Mvua Mkubwa ya Hivi Karibuni ambazo zimeanguka baadhi ya Kutra zake.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Haji Juma Haji aliyevaa shati ya Drafti na Kofia kati kati akimfahamisha Balozi Seif Kulia yake kadhia iliyowapata baadhi ya wananachi waliangukiwa na kuta za nyumba zao ndani ya Mkoa huo.Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja Mstaafu Juma Kassim Tindwa na mbele yao ni Bwana Khamis Haji Machano aliyebomokewa na Nyumba yake Hapo Kijiji cha Pitanazako Kizimbani.
Balozi Seif akimkabidhi Saruji, Matofali na Mchanga Bwana Khamis Haji Machano ikiwa ni mchango utakaomsaidia kuanza matengenezo mengine ya nyumba yake.
Balozi Seif akimfariji na kumpa Pole Mzee Tanzilu Waziri Muharizo wa Kijiji cha Pitanazako Geuni Kikombe Tele baada ya ukuta wa Nyumba yake kubomoka kutokana na Mvua kubwa za hivi karibuni.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi mchango wa Fedha Taslim Bibi Tatu Simai Ali wa Kijiji cha Upenja baada ya kuta za nyumba yake kubomoka kufuatia Mvua kubwa za Masika.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- Taslim zilizotolewa na Waziri wa Nchi OIfisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma Mh. Haroun Ali Suleiman kutekeleza ahadi aliyoitoa kwa Kikundi cha Ushirika cha Saccos cha Kijiji cha Upenja.
Baadhi ya Wanachama wa Saccos ya Kijiji cha Upenja wakisikiliza nasaha za Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif hayupo pichani wakati akikabidhi ahadi ya fedha zilizotolewa na Waziri Haruon Ali Suleiman.(Picha na OPMR – ZNZ.)

Na.Othman Khamis. OMPR. 
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Wananchi wake katika kuona changamoto na matatizo yanayowakumba Wananchi hao ikiwemo majanga na Maafa  yanapatiwa ufumbuzi wa uhakika kadri hali ya uwezeshaji itakavyoruhusu.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi alieleza hayo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua Nyumba zilizopata athari kutokana na kuanguka kwa baadhi ya kuta zake kufuatia Mvua kubwa za Masika zilizonyesha hivi karibuni.

Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Uongozi wa Serikali pamoja na wa  Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja alikabidhi mchango wa Matofali, Saruji, Mchanga na fedha taslimu ikiwa ni hatua ya kutoa mkono wa pole kwa Wananchi waliopatwa na maafa ya kubomokewa kwa Nyumba zao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni