Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza katika Mkutano wakujadili Amani hapa nchini ulioandaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere leo jijjini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim akizungumza katika Mkutano wa Amani ulioandaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere leo jijjini Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Taricisius Ngalalekumtwa mara baada ya kufika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo walikusanyika na baadhi ya wazee na Viongozi wastaafu kuzungumzia Msakabari wa Amani hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa akiteta jambo na Mwenyekiti wa chama cha Wananchi Taifa (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia wakiwa kwenye mkutano wa Amani ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, James Mbatia akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutoka nje ya mkutano wa kujadili Amani hapa nchini uliofanyika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano wa kujadili Amani ulioandaliwa na Tasisi ya Mwalimu Nyerere uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijjini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni