Jumanne, 19 Mei 2015

ELISA MOLLEL ATANGAZA KURUDI TENA ARUMERU MAGHARIBI.

SAM_2626Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa kipindi cha miaka 15 kwa tiketi wa CCM,Elisa Mollel akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kuwa Mbunge jimbo la Magharibi
SAM_2643Mwaandishi wa habari mwandamizi wa gazeti la Mwananchi kulia Mosses Mashala akifanya mahojiano na aliyewahi kuwa mbunge jimbo la Arumeru Magharibi Elisa Mollel,kulia ni anayetajwa kuwania jimbo la Arusha mjini Victor Njau
SAM_2621“Elisa Mollel anasema yuko fiti kiafya na kuhusu watu kusema kuwa ni mgonjwa ni propaganda tu sasa kuingia ulingoni kupambana”
 
Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Arumeru Magharibi kwa tiketi wa CCM,Elisa Mollel ametamka ya kwamba atatangaza uamuzi wa kugombea jimbo hilo au la pindi muda utakapowadia kwa kuwa ana uzoefu mkubwa na siasa za jimbo hilo.
 
Mbali na kauli hiyo Mollel amesema kuwa kwa muda mrefu amekuwa akifuatwa na makundi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa mila maarufu kama Malaigwanani,viongozi wa dini,wakinamama wakimshawishi agombee ubunge mwaka huu.
 
Hadi sasa makada mbalimbali kupitia CCM wilayani Arumeru Magharibi wametangaza nia ambao ni Mathias Manga,Robinson Meitinyiku,Thomas Ole Sabaya pamoja na mbunge wa sasa wa jimbo hilo,Goodluck Ole Medeye.
 
Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Arusha Mollel alisema kuwa tangu alipong”atuka katika utumishi wake baadhi ya wananchi wilayani humo wamekuwa wakimfuata na kumtaka achukue fomu kwa madai mambo hayaendi sawa.
 
“Wananchi wananifuata na kuniambia mzee mambo ni hovyo tangu ulipoondoka,nimefuatwa na makundi mengi tu na mimi nasema muda ukifika nitasema jambo”alisema Mollel
 
Hatahivyo,alisisitiza ya kwamba tangu ang”atuke miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa yakimsikitisha ni pamoja na ubovu wa miundombinu,kero ya maji sanjari na kero ya migogoro ya ardhi matatizo aliyodai yameshindwa kutatuliwa na mrithi wake.
 
Hatahivyo,alisema kuwa miongoni mwa mambo ambayo anajivunia hadi sasa ni pamoja na rekodi yake ya kuboresha sekta ya elimu wilayani humo ambapo aliondoka huku akiwa amefanikiwa kuacha shule za sekondari 26 tofauti na alipoingia madarakani.
 
“Hapo awali tulikuwa na watoto wengi sana wanamaliza elimu ya msingi lakini hawaendi sekondari nimeondoka na kuacha shule za sekondari 26 katika kila kata najivunia kwa hili”alisema kwa kujiamini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni