Ijumaa, 29 Mei 2015

Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka azindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) jijini Arusha

 Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka akizungumza wakati akizindua Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) jijini Arusha leo,kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa NHIF,Michael Mhando na kulia ni Makamu Mwenyekiti  aliyechaguliwa wa Baraza la Wafanyakazi,Deudedit Rutazaa.
 Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya nchini(NHIF),Michael Mhando akitoa hotuba yake leo wakati wa mkutano wa uchaguzi na uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa mfuko huo.
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Taifa,Deusdedit Rutazaa akizungumza baada ya kuchaguliwa na kuhaidi kutoa utumishi uliotukuka.
 Baadhi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)wakiimba wimbo wa Mshikamano kuhamasisha umoja na  maslahi bora kazini.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Wajumbe wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) wakifatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
 Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya NHIF.
Waziri wa Kazi na Ajira,Gaudensia Kabaka(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Mameneja wa mfuko wa  NHIF.

MISHAHARA YA WALIMU KUONGEZWA AGOSTI

87df3-jkNa ,Arusha.
Raisi Jakaya Kikwete amesema kuwa walimu watarajie nyongeza ya mishahara itakayoanza mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni moja kati ya jitihada za serikali katika kuboresha maslahi ya walimu nchini.

Kikwete akihutubia Mkutano Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT ) uliofanyika jijini Arusha jana amesema kuwa nyongeza hiyo itahusisha walimu wote wanaolipwa kima cha chini  cha mshahara na kima cha juu pasipo kutaja kiwango kilichoongezeka.

“Wakati mnachukua mishahara yenu benki mwezi Agosti mtaona tofauti ambayo ni nyongeza ya msahara ,wenzenu wa chama cha Wafanyakazi waliniomba nisitangaze  niongeze kimya kimya ili wafanyabiashara wasipandishe bei ya bidhaa” Alisema Raisi Kikwete

Aidha Raisi Kikwete alisema kuwa serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa inaboresha elimu nchini ikiwa ni pamoja na kuboresha maslahi ya walimu nchini,kuongeza vifaa vya kujifunzia na kufundishia,nyumba za walimu,vitabu  na maabara.

Amesema kuwa madai ya walimu wanayoidai serikali yatalipwa kwa awamu iwapo uhakiki utakamilika kwa sasa wanatarajia kulipa kiasi cha shilingi bilioni 7 kwa walimu 70100 watalipwa Agosti mwaka huu.

“Katika kufanya uhakiki wa madai ya walimu ikiwemo malimbikizo ya mishara,posho za kufundishia,uhamisho tuligundua kuwa wako baadhi ya watu walifanya udanganyifu lakini sasa tunamalizia kufanya uhakiki ili fedha hizo zilipwe” Alisema Kikwete

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Alhaji Yahaya Msulya amemtaka Raisi Kikwete kushughulikia suala la posho ya kufundishia kwa walimu kwani walimu ni kundi linalofanya kazi kwa muda mrefu kuliko watumishi wengine wa serikali.

“Mwalimu anaingia shuleni saa 1:30 asubuhi anatoka saa 3:00 mda huo anatakiwa kusahihisha kazi za wanafunzi na kuandaa masomo ya kufundisha kesho hivyo anatumia muda mwingi sana katika kazi ni vyema serikali ikaliangalia suala hili” Alisema Katibu huyo

Katibu huyo ameupongeza uamuzi wa serikali kutoa bure elimu ya msingi na sekondari ambao utawasaidia watoto wengi hasa waliotoka kwenye familia zenye kipato cha chini.

MITAZAMO HASI KITAMADUNI CHANZO CHA MAUAJI YA WATU WENYE ALBINISM

DSC_0569

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues, akiwasilisha mada katika warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) yanayoendelea nchini yanatokana na mitazamo hasi kitamaduni miongoni mwa wanajamii.
Hayo yameelezwa na washiriki wa warsha ya siku tatu inayoendelea katika kijiji cha Nyakahungwa kata ya Nyakahungwa wilayani Sengerema yenye lengo la kubadili mitazamo iliyojengeka katika jamii na kusababisha madhara makubwa kwa watu wenye albinism iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Warsha hiyo ni miongoni mwa mlolongo wa warsha nne zitakazofanyika katika wilaya za Sengerema, Mwanza, Kahama na Bariadi kwa kuzishirikisha jamii kuibua masuala mbalimbali yanayobagua, kunyanyapaa na kuwatenga watu wenye albinism katika maeneo husika.
Warsha hizo zinafanyika katika kipindi ambacho kumetokea mauaji ya mtoto wa kike, msichana na kijana wenye albinism wilayani Sengerema wakati tarehe 14 Mei 2015 mwanamke mmoja alikatwa mkono wilayani Bariadi.
DSC_0522
DSC_0532
Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Sengerema, Bw. Bushaija Vicent (kulia), akitoa takwimu za idadi ya za wanafunzi wenye albinism katika wilaya yake kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi. Zulmira Rodgrigues.
Kwa mujibu wa Afisa Maendeleo Jamii wilayani Sengerema Bwana Bushaija Vicent kati ya shule za msingi 191 wilayani humo ni Shule zenye watoto wenye albinism ni 14, Idadi yao ni 16 katika shule ya awali watoto 4 wana albinisim, vyuo mbalimbali Sengerema vijana 4 wana albinism na katika Shule za sekondari 48, watoto wenye albinism 4.
Akitoa mada kuhusu uhamasishaji jamii katika masuala ya albinism, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO Bi Zulmira Rodgrigues amesema miongoni mwa masuala ambayo warsha italenga ni kutafakari kwa kina kwa nini watu wenye albinism wanauawa, kubaguliwa, kutengwa na mambo yanayosababisha Tanzania kuongoza katika mauaji hayo ikilinganishwa na nchi nyingine ambazo pia zina watu wenye albinism.
"Watu wenye albinism hawauwawi katika sehemu nyingine duniani, kwa nini Tanzania? Ikiwa mauaji hayo yako kwa wingi nchini Tanzania basi kuna tatizo kubwa ambalo linatakiwa kufanyiwa kazi, na si serikali, UNESCO wala taasisi yoyote ambayo inaweza kuleta mabadiliko hayo isipokuwa jamii yenyewe," alisema Rodrigues.
Tatizo kubwa lililotajwa kuhusiana na mauaji ya watu wenye albinism ni utamaduni uliojengeka katika fikra za watu na kuwa na imani kwamba watu wenye albinism si watu wa kawaida, hawana hadhi na hawastahili kuishi.
Watu wenye albinism ni watu wa kawaida wanaostahili heshima na kulindwa kama binadamu wengine kulingana na kanuni na sheria za nchi na za kimataifa zinazopinga ubaguzi wa rangi, jinsia, tabaka na kukatisha maisha ya mtu. Tofauti ni kwamba rangi yao inatokana na ukosefu wa vinasaba asili vijulikanavyo kama melanin, vyenye uwezo wa kuzalisha rangi ya nywele, macho na ngozi.
Utamaduni uliojengeka katika jamii wa kuwabagua, kuwatenga na kuwapuuza watu wenye ulemavu wa ngozi kumehalalisha mauaji ambayo kwa hivi sasa imekuwa biashara ya kuuza viungo vya watu wenye albinism kwa waganga wa asili kwa lengo la kupata utajiri, cheo na madaraka.
"Mara nyingi waganga wa asili wamekuwa wakitajwa kuwa ndio chanzo cha mauaji hayo kwa ajili ya imani potofu ya kujipatia utajiri, vyeo na madaraka. Biashara hiyo inaonekana kushamiri kwa kuwa hakuna mifumo mahsusi kudhibiti maafa hayo," alisema mmoja wa washiriki anayeshughulikia masuala ya usalama.
DSC_0545
Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi. Rose Haji Mwalimu, akichangia mada kuhusu ushirikishaji jamii katika kuandaa na kutekeleza mikakati itakayochangia kuzuia na kutokomeza unyanyasaji na dhulma zinazofanywa dhidi ya watu wenye albinism iliyoshirikisha waganga wa asili, wauguzi na wakunga, viongozi wa dini, walimu pamoja na watu maarufu iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). Katikati ni Mratibu ambaye pia ni Afisa Mradi wa Elimu ya Afya na VVU/UKIMWI kutoka UNESCO, Bw. Herman Mathias na Kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues.
Akichangia mada wakati wa majadiliano yanayokusudiwa kuzalisha mikakati ya kukomesha maovu hayo, Mratibu na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO Bi Rose Haji Mwalimu alisema kwamba wakati umefika wa kutambua kitu gani kizuri katika tamaduni zilizopo zitakazoweza kusaidia kuleta mafanikio na kuachana na zile ambazo hazina tija na zinasababisha maafa katika maendeleo na ustawi wa jamii.
"Ni kweli kuna changamoto nyingi katika jamii zinazosababishwa na kuhalalisha tamaduni zinazolenga kupotosha badala ya kujenga. Tukiendelea kuzikumbatia tutajikuta tunajenga taifa lisiloona mbali kimaendeleo kuhadaiwa na watu wenye ubinafsi kutoka nje na ndio maana Tanzania imekuwa soko kubwa au shamba lenye rutuba ya kupandikiza mbegu ambazo mavuno yake hupatikana kwa urahisi", alisema Bi Mwalimu.
Katika warsha hiyo washiriki walibaini maeneo makuu matatu ya kuyawekea mpango kazi. Maeneo hayo ni Kuzuia mauaji, ubaguzi, unyanyapaa na kuwatenga, eneo la pili ni kuwalinda watu wenye albinism katika maeneo ya makazi, mashuleni, katika jamii na familia zao na la tatu ni hatua za kisheria wale wote watakaoonekana kuhusika moja kwa moja au kwa namna nyingine katika kuwatendea maovu watu wenye ulemavu wa ngozi kuanzia ngazi za kimataifa, kitaifa, kifamilia na shuleni.
DSC_0553
Mganga wa jadi kutoka kijiji Nyanzenda, wilayani Sengerema, Maimuna Musa akizungumzia jinsi anavyotoa huduma za kutibu watoto magonjwa mbalimbali ya watoto ikiwemo na huduma ya kuzuia mwanamke asizae mtoto mwenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0549
Mganga wa jadi kutoka kijiji cha Nyakasungwa, Omary Mongongwa akitoa msimamo kuhusu uwezo wa tiba kwa waganga wa jadi unavyotofautiana na kuwasihi waganga wenzake wa jadi wanapojadili wazungumzie kazi za mtu binafsi na utendaji wake na si kuusemea moyo wa mganga mwingine.
DSC_0596
Mzee maarufu kutoka kijiji cha Bukokwa, Felician Buhumbi, akifafanua hatua zilizokuwa zikichukuliwa wakati wa Ukoloni dhidi ya waganga asili wenye kupiga ramli chonganishi wakati wa warsha ya siku tatu iliyofanyika katika kijiji cha Nyakahungwa wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
DSC_0511
Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo ya siku tatu iliyowashirikisha, Waganga wa Jadi, Viongozi wa dini, walimu shule za msingi na sekondari, wazee maarufu, Wakunga, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Shirika la Under the Same Sun, Baraza la taifa la dawa asilia, Afisa wa polisi wa dawati la jinsia pamoja na Maafisa wa mkoa wa Mwanza na wa wilaya ya Sengerema.
DSC_0652
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini, Bi. Zulmira Rodgrigues aliyeambatana na mbunge wa viti maalum CCM anayetetea maslahi ya watu wenye albinism, Mh. Al-Shaymaa Kwegyir wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki.

FAMILIA YA MTOTO ALIYEGONGWA NA GARI NA KUKATWA MIGUU YAOMBA MSAADA

Naibu Kamanda wa UVCCM ,Innocent Melleck akiwa na mama mzazi wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima mara baada ya kukabidhi kiti cha walemavu cha magurudumu kwa ajili ya kusaidia kutoka eneo moja hadi jingine.
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi vijijini ,Innocent Melleck akikabidhi Pempers kwa mama wa mtoto Felista ,Beatrice Shirima kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo aliyepata ulemavu wa miguu miwli baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso.
Naibu kamanda wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini ,Innocent Melleck akiwa amembeba mtoto Felista Shirima(3) aliyekatwa miguu yote miwili baada ya kugongwa na gari aina ya Fuso jirani na nyubani kwao.

Akizungumzia sakata la mtoto huyo Naibu kamanda huyo alisema kuwa ataumia kila aina ya uwezo na nguvu zake kwa kushirikiana na ofisi ya umoja wa vijana wa chama chama mapinduzi UVCCM ili kuhakikisha kuwa  haki ya mtoto huyo inapatikana.
Awali akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msaada wa baiskeli  ya magurudumu matatu na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki saba na kamanda huyo, mama mzazi wa mtoto huyo Beatrice Kelvin,aliiomba serikali na wadau mbalimbali kujitokeza na kumsaida mwanae ili kuhakikisha haki inapatikana. 

Alisema kesi iliyokuwepo mahakama kwa ajili ya kudai haki za msingi za mwanae imeisha bila haki yake kupatikana licha ya kuhangaika sehemu mbalimba na kuomba vyombo husika vinavyo jishughulisaha na haki za binadamu kuingilia kati suala hilo hatua ambayo itasaida kupata haki.

WATANZANIA WAMETAKIWA KUONDOKANA NA FIKRA POTOFU JUU YA UGONJWA WA FISTULA


Watanzania nchini wametakiwa kuachana na fikra potofu za kuamini kuwa
ugionjwa wa fistula kwa wanawake unasababishwa na kuwa na mahusiano ya
kingono na wanaume wengi ama kulogwa kwani ugonjwa huo unasababishwa na
kuchwelewa kwa mama mjamzito kujifungua hivyo kusababisha tundu ambalo
humletea athari za kiafya.



Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Maternity Afrika, Paulo
Letura ,Amesema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na umbali mrefu wa vituo vya
afya kwa kina mama wajawazito hivyo amewataka kina mama kuwahi katika vituo
vya afya na kujifungua katika vituo hivyo badala ya kwenda kwa wakunga wa
jadi.



Paulo Letura amesema kuwa kwa sasa wanafanya juhudi za kutoa elimu hasa
maeneo ya vijijini  ambako uelewa ni mdogo na kuwataka wajawazito wafike
mapema kwenye vituo vya afya kwa kuchelewa kunasababisha msuguano wa mtoto
tumboni ambao husababisha tundu karibu na kibofu cha mkojo na karibu na
utumbo mkubwa.



Letura alisema hayo jana wakati wakitoa masaada wa kitaalamu wa matibabu na
upasuaji kwa kina mama pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu.





Mkurugenzi wa shirika hilo ambaye ni Daktari aliyebobea katika ugonjwa huo
Dr.Andrew Browing anasema kuwa wamekua wakifanya kazi na vituo mbalimbali
vya afya ikiwemo KCMC,CCBRT katika kuhakikisha kuwa wakinamama wanapata
tiba ya ugonjwa huo hivyo amewashauri kinamama wajitokeze kupata matibabu
badala ya kukaa nyumbani.



Kwa upande wake Mtaalamu wa Afya katika shirika hilo Paivi Karlssom
amewataka kina mama kujenga utamaduni wa kujifungulia katika vituo vya afya
ili wapate msaada wa kitaalamu badala kujifungulia kwa wakunga wa jadi.



Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani  (WHO) Wanawake na
wasichana 3000 wanapata tatizo hili  wenye umri kati ya miaka 22 hadi 24
hupatwa na tatizo hili zaidi.

UMOJA WA WATANZANIA WALIOSOMA NCHINI AUSTRALIA WAZINDULIWA RASMI

 Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Watanzania  waliosoma nchini Australia wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (kushoto) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) leo jijini Dar es Salaam.
Add caption
  Waziri wa Afya na Utalii wa Australia Mh. Dkt. Kim Hames akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) jijini Dar es Salaam leo.
 Rais wa Umoja wa Watanzania waliosoma nchini Australia (TAAA) Bw. Francis Mhimbila akizungumza wakati wa uzinduzi wa Umoja huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Bw.Mathias Kabunduguru (aliyesimama) aliyemuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi Mh. Celina O. Kombani (Mb) akizungumza na Watanzania walionufaika na ufadhili wa masomo nchini Australia.

Maadhimisho ya SIKU YA AFRIKA yafanyika Washington DC

Balozi wa Misri nchini Marekani Mhe. Mohamed Tawfik akiongea kufungua sherehe ya African Union iliyofanyika siku ya Alhamisi May 28, 2015 katika hotel ya JW Marriott, Washington DC
Balozi wa Morocco nchini Marekani Mhe. Rashad Bouhlal akiongea machahce.
Msemaji mkuu wa sherehe ya siku ya Afrika Mhe. Donald Tetelbaum.
Mchungaji Jesse Jackson akiongea kwenye sherehe ya siku ya Afrika.

Maureen Umeh mfanyakazi wa kituo cha luninga cha Fox News DC akisherehesha sherehe ya siku ya Afrika.
Mambalozi wa Afrika nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba.
Mkuu wa Utawala na Fedha mama Lily Munanka akisalimiana na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Githae.

WANAHABARI MKOA WA IRINGA NA POLISI WAKUTANA KATIKA KIKAO CHA MAHUSIANO MEMA

Baadhi ya wanahabari  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika picha  ya pamoja na viongozi  wa  jeshi la polisi mkoa wa Iringa mara baada ya  kumalizika  kikao  chao cha mahusiano mema na kutambulishana kati ya wanahabari na viongozi wapya wa  jeshi  la Polisi waliokaa ni kamanda wa polisi Ramadhan Mungi wa tatu  kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard na katibu wa IPC Francis Godwin na maofisa wengine wa polisi mkoa
Baadhi ya askari polisi wakiwa ktk kikao cha pamoja na wanahabari leo
Wanahabari Mkoa wa Iringa wakiwa ktk kikao cha pamoja na maofisa wa jeshi la Polisi




Wanahabari  wakiwa katika kikao na jeshi la polisi
Kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi akitoa mafunzo mafupi kwa  wanahabari kati ya utendaji kazi wa  jeshi la polisi na vyombo vya habari

 Na FG BLOG
Wanahabari wa mkoa wa Iringa leo wamekutana na kamanda wa polisi na maofisa wa jeshi la polisi Mkoani hapa ili kuendelea kufanya Kazi kwa ushirikiano kwa faida ya Mkoa wa Iringa.

Katika kikao hicho kilichoambatana na semina fupi ya kukumbushana wajibu wa Kazi za wanahabari na askari.

Akitoa mafunzo hayo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa ili kuufanya Mkoa wa Iringa uweze kufanikiwa ni lazima wabahabari na polisi kufanya Kazi zao kwa kuzingatia maadili na kutofanya upendeleo katika utendaji wao.

Mungi alisema kuwa mbali ya kazi kubwa ambazo vyombo vya habari mkoani hapa vinafanywa bado jeshi lake limeamua kukutana na wanahabari hao ili kizidi kuufanya Mkoa kuwa na taswira nzuri ktk mahusiano Kati ya pande hizo mbili kama njia ya kuwatumikia wananchi.

Alisema kwa Mkoa wa Iringa vyombo vya habari vimeonyesha mchango mkubwa zaidi zaidi na kutaka mchango huo na jitihada hizo kuendelea zaidi .

Kamanda Mungi amesema kuna haja ya wanahabari na askari polisi kuendelea kujenga mahusiano kwa kukutana na viongozi wao kabla ya kufanya mapambano yasiyo na tija.

Alisema kuwa wao kama jeshi la polisi wanatambua kuwa vyombo vya habari ni muhimu kwa jamii hivyo lazima kujenga mahusiano mema na kuwa askari polisi hawanasababu ya kuendeleza mivutano 

Alisema kuwa kuna wakati mwingine ajali imetokea na Kazi ya mwanahabari ni kuhabarisha umma na polisi kuokoa hivyo lazima kufanya Kazi kwa karibu na kutoa majibu stahiki kwa wanahabari na wanahabari kutotumia jazba katika utendaji Kazi zao 

Akizungumza katika mafunzo hayo  mwenyekiti wa chama cha  waandishi  wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard  alisema  kuwa hatua ya  jeshi la polisi mkoa wa Iringa kuandaa kikao  hicho cha kufahamiana na mafunzo mafupi kwa wanahabari ni ya kupongezwa zaidi hasa kwa wakati  huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu .

Alisema  kuwa tofauti baina ya badhi ya askari na wanahabari  ilikuwa ikijitokeza kutokana na pande  hizo  mbili zinazofanya kazi za kijamii kutoatambuana vilivyo hivyo kila upande  kuonyesha chuki dhidi ya mwingine jambo ambalo halijengi bali hubomoa.

Leonard  alisema kikao  hicho  kina umuhimu mkubwa kwa wanahabari  hasa  wakati  huu  wa kuelekea  uchaguzi mkuu ambao baadhi ya askari  walikuwa  wakiwachukia wanahabari na  wanahabari  kuwachukia polisi hasa kutokana na matukio ya nyuma kabla ya Mungi  kuwa kamanda wa  polisi wa mkoa huo wa Iringa.

Katika  hatua  nyingine mwenyekiti  huyo aliomba  jeshi la polisi  kuwa  na utaratibu wa kukutana na  wanahabari japo kwa  mwezi mara moja  ili  kujitathimini  utendaji kazi wao na  pale  penye tofauti  basi  kuweza kuzimaliza kwa njia  sahihi kuliko kila mmoja kutumia nguvu zisizo na tija.