Mjumbe
Mkutano Mkuu wa CCM Manispaa ya Singida, Hasan Mazala akionesha vijana
fomu yake ya kuwania ubunge Jimbo la Singida Mjini jana kwenye ukumbi wa
mikutano wa CCM Mkoani Singida.
Mazala akiwaasa vijana kufanya kazi kwa nguvu katika jimbo hilo.
Mkinipa nafasi ya kuwatumikia mambo yatanyooka namna hii.
Mgombea
wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Singida Mjini Hassan Philipo Mazala
akisistiza jambo kwa vijana waliomsindikiza kuchukua fomu.
Baadhi
ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja na Hassan Mazala nje ya jengo
la makao makuu ya CCM Mkoa wa singida mara baada ya kuchukua fomu.(PICHA
ZOTE NA HILLARY SHOO).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa
(MNEC) Manispaa ya Singida,Hassan Mazala amechukua fomu ya kuwania
Ubunge Jimbo la Singida Mjini ..
Akizungumza na kundi la Vijana wa
CCM kwenye ukumbi mdogo jana, Mazala amesema kuwa amefungua ukurasa mpya
wa maisha yake kwa kuwania nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Mohammed
Dewji aliyestaafu.
‘Nimejipima nikaona ninaweza kuvaa
viatu vilivyoachwa wazi na Dewji kwani katika kipindi chote alichukuwa
Mbunge nilishirikiana nae katika kuyatekeleza yale yote aliyonituma kama
msaidizi wake wa karibu.” Alisema Mazala.
“Nimekuwa Kiongozi kwa muda mrefu
katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye vijiji ,Kata, Wilaya, Mkoa na
sasa Taifa, hivyo nina uwezo wa kutosha na nimekomaa kisiasa katika
kufanya kazi hii ya Ubunge bila wasiwasi wowote pale alipoachia Dewji”
Alisisitiza.
Aidha alisema anazifahamu changamoto
zinazolikabili Jimbo hilo kwani ametembea kona zote na kujionea hali
halisi ya wananchi wanavyojishigulisha na shughuli za kijamii.
“Nina Moyo wa dhati kabisa wa
kuwatumikia, ninaombeni mnibebe, najua yamesemwa mengi sana juu yangu
katika kipindi ambachio nimlikuwa nafanya kazi na MO, lakini yapuuzeni
hayo kwani hayana ukuweli wowote ni chuki binafsi tu.” Alisema huku
akishangiliwa na kundi la vijana linalojiita team Mazala.
Hata hivyo Mazala ambaye ana uwezo
mkubwa wa kutawa jukwaa alisema kamwe hatawaanguisha wananchi wa Jimbo
hilo huku akitumia misamiati Zimwi likujualo, Usiache mbachao na mwokoto
kuni porini huota moto pamoja.
Akitangaza kutogombea tena Ubunge
mapema Julai 08 mwaka huu mjini Singida Dewji alimsifu Mazala kwa kusema
kuwa ni mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu na ana moyo wa kujitolea
kwani aliweza kusimamia kazi zake zote bila ya matatizo yoyote.
“Na pia ninapenda kumshukuru kipekee
mtu mmoja ambaye bila yeye mafanikio yangu ya kiuongozi niyoyopata hapa
Singida yasingeweza kufanikiwa vizuri bila ya yeye.” Alisema Dewji
katika taarifa yake hivi karibuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni