Ofisa
Mauzo wa Airtel, Salma Juma akimuelekeza jambo Mtangazaji wa Kituo cha
Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde kabla ya kumsmartfonika simu ya
kisasa mapema wiki hii katika duka la wazi la Airtel lililopo Game
Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa
Airtel, Aneth Muga.
Meneja
Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kulia), akimsmartfonika simu Mtangazaji
wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde.
Ofisa
Mauzo wa Airtel, Rehema Hoza (katikati), akimkabidhi Kibonde kifaa cha
kutunzia umeme 'Powerbank'. Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga.
Meneja Mawasiliano wa Airtel, Jackoson Mmbando, akimuelekeza jambo, Kibonde baada ya kusmartfonika simu hiyo ya kisasa.
Ofisa
Mauzo wa Airtel, Eveline Amos (kushoto), akiwaelekeza jambo, Kibonde na
mteja mwingine waliofika katika duka la wazi lililopo Game Mlimani
City.
Maofisa Mauzo wa Airtel wakiwahudumia wateja katika duka hilo la wazi.
Maofisa mauzo wa Airtel wakiwa katika duka la wazi Game Mlimani City.
Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakiwa duka la wazi Game Mlimani City.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Simu ya Airtel imeendelea kuwa smartfonika watu maarufu kwa
kuwapatia zawadi za simu kwa awamu tofauti kama walivyojiwekea utaratibu
huo.
Akizungumza na mwandishi wa habari Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema kwa wiki hii mpango huo wa
smartfonika umemdondokea Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds,
Ephrahim Kibonde ambapo amepata zawadi ya simu ya kisasa yenye uwezo
mkubwa.
"Tumejipanga
vizuri katika mpango huu wa kuwasmartfonika watu maarufu wakiwemo wa
sanii na wadau mbalimbali katika wakati tuliopanga" alisema Mmbando.
Mmbando
alisema pamoja na kuendelea kuwasmartfonika walengwa hao sasa mpango
mzima utakuwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza
mapema wiki hii katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar
es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni