Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni
ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki Maonyesho ya Biashara
ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na
Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi
unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zishakamilika.
Aliongezea
kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata
ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la
Kigamboni.
Mradi
huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza
zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na
apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment
zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani
ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote
kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi,
hospitali, supermarket, na kadhalika.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village akimhudumia wateja wao aliyefika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Muonekano wa Banda lao lililopo viw
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village akimhudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village (katikati)
akiwaonyesha wafanyakazi wa kampuni hiyo namna walivyoweza kufanya vyema
katika mauzo ya nyumba.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni