Alhamisi, 2 Julai 2015

AIRTEL YAINGIA MKATABA NA FINCA WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa Airtel na Finca kutoa huduma za kifedha. Kutoka kulia ni , Vivian Temi na Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea.
 Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu huduma hiyo. Kulia ni Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.


Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa.








 Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa akizungumza katika mkutano huo. 


 Maofisa wa Airtel na Finca wakionesha bango wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania imesaini makubaliano na benji ya Finca Microfinance kwaajili ya kuwezesha wateja kuzifikia pesa zao kirahisi kwa kupitia simu zao za mkononi.

Huduma hiyo mpya itawawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money na kutoa kwenye simu kwenda benki.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema huduma hiyo inalenga kuwawezesha wateza wao kufanya miamala yao mbalimbali ya kifedha wakati wowote kwa usalam azaidi.

Alisema kwa kutambua finca sasa ni taasisi ya kibenki wameona ni vyema kuungana na kuweza kutoa huduma za kuhamisha pesha kwa usalama na kwa ghalama nafuu kupitia simu za mkononi kwa wateja wao nchi nzima.

"Airtel itaendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia mahitaji ya wateja wake kwa kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali katika kuboresha huduma zao kwa wateja," alisema.

Naye Meneja wa Kanda wa Finca Microfinance Benki, Sarah Daffa alisema huduma hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi kwenye huduma zao.

"Tunawashukulu Airtel kwa kuungana nasi kupitia huduma za Airtel Money, tunaimani ushirikiano utatuwezesha kuongeza idadi ya wateja wetu tu bali utasaidia kuongeza idadi ya miamala inayofanyika kwa urahisi na salama," alisema.

"Wateja wetu sasa wataweza kufanya miamala ya pesa wakati wowote mahali popote mara nyingi zaidi ikiwa tu watasajiliwa kweye huduma hiyo na akaunti yake ya benki ikiwa hai," alisema.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni