Bia za Windhoek zinavyoonekana.
Mshauri
wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits
Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam
jana kuhusu kupinga uamuzi wa tume ya ushindani (FCC) na kuidai fidia
hiyo ya sh. tirioni moja kutoka na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia
ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania ki holela.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo
Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira (katikati),
akizungumza katika mkutano huo na kusema bia halali iliyopo kwenye soko
ni ile yenye namba MB 66 na inayosambazwa na kampuni hiyo. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Mabibo, Anic Kashasha na Wakili,
Stephano Kamala.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kampuni ya Mabibo, Anic Kashasha (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Wakili wa Kampuni hiyo, Respicious Didace na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira.
Wakili, Stephano Kamala (kulia), akizungumza katika
mkutano huo.
Meza Kuu. Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Mabibo,
Alice Marco.
Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo.
Mdau Faustine Kapama akiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambayo ni wasambazaji wa bia ya
Windhoek inaidai Tume ya Ushindani (FCC), sh.tirioni 1 kwa kukiuka
uhalali wa mkataba wa Mabibo na kudai unapingana na ushindani.
Katika
hatua nyingine kampuni hiyo imeiomba Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi
kuhusu uhalali wa uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Ushindani (FCT)
mwezi Aprili 2015 kuhusu haki ya Mabibo ya kuagiza na kusambaza bia za
Windhoek kipekee katika soko la Tanzania.
Hayo
yalibainishwa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya
Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira wakati akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.
Alisema
mwezi Aprili 2015, FCT ilitoa uamuzi ambao ni sawa na kutangaza kuwa
mkataba kati ya Mabibo Beer Wines and Spirits na Namibia Breweries
Limited uliosajiriwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na
Huduma wa kipee wa Mabibo haukuwa halali kisheria.
"Si
FCC wala FCT yenye mamlaka yakutengua uamuzi halali wa Mahakama
kutafsiri sheria na katiba ya Tanzania. Katika kufungua shauri lake
katika Mahakama ya Rufaa tarehe 24 Juni 2015, Mabibo imeiomba Mahakama
kuthibitisha kwamba mwenendo wa Mabibo ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya
Ushindani ya mwaka 2003, kama Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni
ilivyoamua mwaka 2010 na kuwa FCC na FCT walifanya kinyume cha mamlaka
zao za kisheria na kikatiba na kujipa uwezo wa kutengua maamuzi ya
Mahakama za Tanzania" alisema Rugemalira.
Aliongeza
kuwa mbali na kuzidisha na kupanua mamlaka yao maamuzi ya FCC na FCT
pia yanapuuza ukweli wa msingi. Wakati Windhoek ni bidhaa maalumu
inayofahamika kimataifa, ambapo mauzo yake nchini ni kiasi cha asilimia
0.05 tu ya soko la jumla nchini na sio kampuni inayotawala soko la bia
Tanzania.
Alisema
Mabibo inataka fidia hiyo kutoka FCC na washirika wake kwa sababu amri
isiyo halali ya FCC imeruhusu muendelezo wa uagizaji wa bia ya Windhoek
na wasambazaji wasioruhusiwa hivyo kuharibu biashara ya Mabibo na mkondo
wa uadilifu wa bidhaa ya Windhoek katika soko la bia Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni