Jumanne, 7 Julai 2015

MTANGAZA NIA UBUNGE LUDEWA AANGUKIA PUA NAFASI YA NEC ,ASEMA HATAKI TENA KUGOMBEA

Aliyeshindwa ujumbe wa NEC Ludewa Injinia Zephania Chaula  akiangana na mbunge  Deo  Filikunjombe baada ya  kushindwa katika nafasi  hiyo ,Chaula alikuwa ni mmoja wa wana CCM waliokuwa  wakitaka kuwania ubunge jimbo la Ludewa
Chaula akiagana na mshindi mzee Nkwera 
 Mkuu  wa wilaya ya  Ludewa Antonia Choya akimkabidhi  hati ya  shukrani mbunge wa Ludewa  Deo Filikunjombe (kushoto)
 Mjumbe  wa  mkutano huo Bw  Choya  akipiga  kura.
 Wajumbe  wakishiriki  kupiga  kura.
 Wajumbe  wakishiriki  kupiga kura
 Mgombe  Chaula  akishukuru kwa  kushindwa
 Injinia  Chaula  akimpongeza mshindi mzee Nkwera.
Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe  akipiga  kura  kumchangua mjumbe wa NEC Ludewa
Na MatukiodaimaBlog
 
MBIO za  ubunge jimbo la  Ludewa  mkoani  Njombe zimeishia hewani  kwa
mtangaza  nia wa  wanafasi  hiyo Injinia  Zephania  Chaula  baada ya
kuambilia  kura 11 pekee katika nafasi ya mjumbe  wa Halmashauri  kuu (
NEC) Taifa kutoka  wilaya ya Ludewa  aliyokuwa akiwania dhidi ya katibu
msaidizi  wa mbunge wa  jimbo la Ludewa  Hilaly  Nkwera  aliyeibuka
mshindi kwa  kupata  kura 138 kati ya  kura  zote halali 151 zilizopigwa .

Huku mgombea  huyo aliyeshindwa katika nafasi hiyo ya Ujumbe wa NEC Injinia Chaula  akiapa  kutogombea tena nafasi hiyo kwa
madai kuwa ni mara ya pili sasa anashindwa  vibaya  katika  mchakato 
wa  kuwania nafasi hiyo ambapo awali alishindwa mgombea  wa darasa  la 
saba marehemu Elizabeth Haule .

Uchaguzi
huo  mdogo  wa  kuziba nafasi ya  mjumbe  wa  NEC  iliyoachwa  wazi na
aliyekuwa  mjumbe wa nafasi hiyo Elizabeth Haule  aliyefariki  dunia
mapema mwaka  huu ,ulifanyika  mwishoni mwa  wiki  hii kwa
kuwashirikisha  wagombea  hao  wawili kabla ya mgombea  mwingine ambae
ni mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe  kuandika barua ya
kujitoa katika  kinyang’anyiro  hicho akiwapisha wagombea  hao
wachuane  kutokana na yeye  kudai  kuwa atachukua fomu ya kugombea tena
ubunge  wa  jimbo  hilo la Ludewa .

Akitangaza
matokeo  hayo ya  uchaguzi msimamizi  mkuu  wa uchaguzi huo  Lucas
Nyanda  ambae ni katibu  wa  jumuiya  ya  wazizi wa CCM mkoa  wa Njombe
,alisema  kuwa  jumla ya  wajumbe  waliopaswa  kushiriki katika
uchaguzi  huo ni 164 ila   wajumbe  halali  walioshiriki ni 151 na kati
ya  wajumbe  hao kura 2  ziliharibika  huku Injinia Chaula akipata  kura
11 na mshindi wa nafasi hiyo Bw  Nkwera  akipata  kura 138
 
Awali
mbunge  wa  jimbo la  Ludewa  Bw  Filikunjombe  ambae alikuwa ni mmoja
kati ya  wana CCM watatu  ambao majina  yao yalirejeshwa  kuwania
nafasai hiyo alisema  kuwa analazimika  kujitoa katika  nafasi hiyo
ili  kupisha wanachama  hao wawili  ambao wamemzidi  umri  ili  kuweza
kupambana  na  yeye ataendelea  kuwa kuwatumikia  wananchi  wa Ludewa
katika nafasi ya  ubunge pekee.


Akiwashukuru wajumbe
kwa ushindi  huo  wa nafasi ya ujumbe wa NEC Bw  Nkwera ambae
kitaaluma ni mwalimu na pia amepata  kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa madiwani wa mkoa wa Njombe na Iringa
alisema kuwa
amefurahishwa na imani  kubwa ambayo wana CCM wameionyesha  kwake  kwa
kumchagua  kuwa mwakilishi wao katika vikao  vya  kitaifa .

Bw
Nkwera  alisema wana CCM Ludewa waamini  kuwa nafasi hiyo hawajakosea
kumpa na kamwe  hatawaangusha kwani atahakikisha anawatumikia  vema
katika vikao  vya  juu kwa kuanza na  safari ya  kumpata mgombea wa
nafasi ya  Urais wa CCM ambae atakuwa ni chaguo la  wana CCM wote wa
Ludewa .
Huku
Chaula mbali ya  kuwashukuru kwa  kura  11 alizopata bado  alisema
kuwa hatakuwa tayari  kuendelea  kugombea tena kwani yawezekana kabisa
Mungu hajapenda  yeye  kuwa  kiongozi wa kisiasa bali ametaka  aendelee
kuwa mtaalam .
“Nasema haya
kutoka moyoni mimi ni mwanachama hai wa chama cha mapinduzi na nakipenda chama change
hivyo naahidi sitagombea tena katika maisha yangu nafasi hii ya UNEC  kutokana
na ukweli kuwa nahisi siasa inanikataa maana kila nikigombea nashindwa hivyo
ngoja nifanye kazi nyingine pia nampongeza  sana mshindi Mzee  Nkwera katika
utendaji wake ndani ya chama”,alisema Mhandisi Chaula

Wakati
huo  huo serikali  ya  mkoa  wa Njombe kupitia mkuu wa mkoa wa Njombe
Dr  Rehema Nchimbi imempongeza kwa  kumpa hati ya shukrani  mbunge  wa
jimbo la Ludewa  Bw  Filikunjombe kwa  ushiriki  wake  mkubwa katika
kufanikisha  mbio  za mwenge katika  mkoa  huo kwa kuwa mbunge  pekee
kushiriki  mbio  za mwenge na kuchangia vizuri .
 
Akikabidhi hadi  hiyo mbele ya  wajumbe wa mkutano wa Halmashauri  kuu , mkuu wa
wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya aliweza kumtunuku hati hiyo ya  heshima mbunge wa
jimbo la Ludewa  Filikunjombe kwa kushiriki kimamirifu katika mbio za
mwenge wa Uhuru ndani ya mkoa wa Njombe.
Akitoa chetihicho Bw.Choya alisema kuwa kutokana na ushiriki alioufanya mh.Filikunjombe
katika mbio cha mwenge wa Uhuru mkuu wa mkoa wa Njombe na ofisi yake wameona
wampatie cheti cha heshima Filikunjombe kwani ni mbunge pekee aliyeshiriki
katika mbio hizo za Mwenge katika mkoa wa Njombe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni