Alhamisi, 2 Julai 2015

AIRTEL YAINGIA MKATABA NA FINCA WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA

 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa Airtel na Finca kutoa huduma za kifedha. Kutoka kulia ni , Vivian Temi na Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea.
 Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu huduma hiyo. Kulia ni Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.


Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa.








 Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa akizungumza katika mkutano huo. 


 Maofisa wa Airtel na Finca wakionesha bango wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania imesaini makubaliano na benji ya Finca Microfinance kwaajili ya kuwezesha wateja kuzifikia pesa zao kirahisi kwa kupitia simu zao za mkononi.

Huduma hiyo mpya itawawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money na kutoa kwenye simu kwenda benki.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema huduma hiyo inalenga kuwawezesha wateza wao kufanya miamala yao mbalimbali ya kifedha wakati wowote kwa usalam azaidi.

Alisema kwa kutambua finca sasa ni taasisi ya kibenki wameona ni vyema kuungana na kuweza kutoa huduma za kuhamisha pesha kwa usalama na kwa ghalama nafuu kupitia simu za mkononi kwa wateja wao nchi nzima.

"Airtel itaendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia mahitaji ya wateja wake kwa kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali katika kuboresha huduma zao kwa wateja," alisema.

Naye Meneja wa Kanda wa Finca Microfinance Benki, Sarah Daffa alisema huduma hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi kwenye huduma zao.

"Tunawashukulu Airtel kwa kuungana nasi kupitia huduma za Airtel Money, tunaimani ushirikiano utatuwezesha kuongeza idadi ya wateja wetu tu bali utasaidia kuongeza idadi ya miamala inayofanyika kwa urahisi na salama," alisema.

"Wateja wetu sasa wataweza kufanya miamala ya pesa wakati wowote mahali popote mara nyingi zaidi ikiwa tu watasajiliwa kweye huduma hiyo na akaunti yake ya benki ikiwa hai," alisema.

KAMPUNI YA MABIBO BEER YAIDAI TUME YA USHINDANI (FCC) SH.TIRIONI MOJA

 Bia za Windhoek zinavyoonekana.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa tume ya ushindani (FCC)  na kuidai fidia hiyo ya sh. tirioni moja kutoka na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania ki holela.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira (katikati), akizungumza katika mkutano huo na kusema bia halali iliyopo kwenye soko ni ile yenye namba MB 66 na inayosambazwa na kampuni hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Mabibo, Anic Kashasha na Wakili, Stephano Kamala.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kampuni ya Mabibo, Anic Kashasha (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Wakili wa Kampuni hiyo, Respicious Didace na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira.
 Wakili, Stephano Kamala (kulia), akizungumza katika 
mkutano huo.
 Meza Kuu. Kushoto ni Meneja wa Kampuni ya Mabibo, 
Alice Marco.
 Maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye mkutano huo.
 Mdau Faustine Kapama akiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambayo ni wasambazaji wa bia ya Windhoek inaidai Tume ya Ushindani (FCC), sh.tirioni 1 kwa kukiuka uhalali wa mkataba wa Mabibo na kudai unapingana na ushindani.

Katika hatua nyingine kampuni hiyo imeiomba Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Ushindani (FCT) mwezi Aprili 2015 kuhusu haki ya Mabibo ya kuagiza na kusambaza bia za Windhoek kipekee katika soko la Tanzania.

Hayo yalibainishwa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana.

Alisema mwezi Aprili 2015, FCT ilitoa uamuzi ambao ni sawa na kutangaza kuwa mkataba kati ya Mabibo Beer Wines and Spirits na Namibia Breweries Limited uliosajiriwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na Huduma wa kipee wa Mabibo haukuwa halali kisheria.

"Si FCC wala FCT yenye mamlaka yakutengua uamuzi halali wa Mahakama kutafsiri sheria na katiba ya Tanzania. Katika kufungua shauri lake katika Mahakama ya Rufaa tarehe 24 Juni 2015, Mabibo imeiomba Mahakama kuthibitisha kwamba mwenendo wa Mabibo ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, kama Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilivyoamua mwaka 2010 na kuwa FCC na FCT walifanya kinyume cha mamlaka zao za kisheria na kikatiba na kujipa uwezo wa kutengua maamuzi ya Mahakama za Tanzania" alisema Rugemalira.

Aliongeza kuwa mbali na kuzidisha na kupanua mamlaka yao maamuzi ya FCC na FCT pia yanapuuza ukweli wa msingi. Wakati Windhoek ni bidhaa maalumu inayofahamika kimataifa, ambapo mauzo yake nchini ni kiasi cha asilimia 0.05 tu ya soko la jumla nchini na sio kampuni inayotawala soko la  bia Tanzania.

Alisema Mabibo inataka fidia hiyo kutoka FCC na washirika wake kwa sababu amri isiyo halali ya FCC imeruhusu muendelezo wa uagizaji wa bia ya Windhoek na wasambazaji wasioruhusiwa hivyo kuharibu biashara ya Mabibo na mkondo wa uadilifu wa bidhaa ya Windhoek katika soko la bia Tanzania.

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA KIKOSI KAZI CHA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KIMAZINGIRA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Katika hotuba yake IGP Mangu aliomba ushirikiano na wananchi katika kupambana na uharibifu  wa mazingira nchini. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Utunzaji wa Mazingira (ICCF) la nchini Marekani, Dk Kaush Arha akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana na uhalifu wa kimazingira kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu nchini. Uuzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Viongozi mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Viongozi mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

AIRTEL SMARTFONIKA YAMFIKIA MTANGAZAJI EPHRAIM KIBONDE WA CLOUDS FM

 Ofisa Mauzo wa Airtel, Salma Juma akimuelekeza jambo Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde kabla ya kumsmartfonika simu ya kisasa mapema wiki hii katika duka la  wazi la Airtel lililopo Game Mlimani City jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga.
 Meneja Masoko wa Airtel, Aneth Muga (kulia), akimsmartfonika simu Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephraim Kibonde.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Rehema Hoza (katikati), akimkabidhi Kibonde kifaa cha kutunzia umeme 'Powerbank'. Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Aneth Muga.
 Meneja Mawasiliano wa Airtel, Jackoson Mmbando, akimuelekeza jambo, Kibonde baada ya kusmartfonika simu hiyo ya kisasa.
 Ofisa Mauzo wa Airtel, Eveline Amos (kushoto), akiwaelekeza jambo, Kibonde na mteja mwingine waliofika katika duka la wazi lililopo Game Mlimani City.
 Maofisa Mauzo wa Airtel wakiwahudumia wateja katika duka hilo la wazi.
 Maofisa mauzo wa Airtel wakiwa katika duka la wazi Game Mlimani City.
 Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
  Wateja wakihudumiwa katika duka la Airtel Mlimani City.
Wateja wakiwa duka la wazi Game Mlimani City.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Simu ya Airtel imeendelea kuwa smartfonika watu maarufu kwa kuwapatia zawadi za simu kwa awamu tofauti kama walivyojiwekea utaratibu huo.

Akizungumza na mwandishi wa habari  Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema kwa wiki hii mpango huo wa smartfonika umemdondokea Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Clouds, Ephrahim Kibonde ambapo amepata zawadi ya simu ya kisasa yenye uwezo mkubwa.

"Tumejipanga vizuri katika mpango huu wa kuwasmartfonika watu maarufu wakiwemo wa sanii na wadau mbalimbali katika wakati tuliopanga" alisema Mmbando.

Mmbando alisema pamoja na kuendelea kuwasmartfonika walengwa hao sasa mpango mzima utakuwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yaliyoanza mapema wiki hii katika viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Mmbando ametumia fursa hiyo kuwataka wateja wa Airtel kutembelea banda lao lililopo katika viwanja hivyo ili kupata huduma mbalimbali pamoja na kujipatia simu za aina mbalimbali kwa bei nafuu

BENKI YA CRDB YAVUTIA WATU WENGI KATIKA MAONYESHO YA SABASABA

BENKI ya CRDB imewataka Watanzania kutembelea banda lao ili kupata huduma mbalimbali za Fedha.

Akizungumza katika Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba, Ofisa wa benki hiyo, John Titus amesema kuwa banda lao linashughulika na kufungua akaunti na kumuhudumia mteja.

Aliongeza kuwa Benki ya CRDB pia imeweka Mobile  Branch ambayo hufanya kazi zote zinazofanywa na benki hiyo ikiwemo huduma za kuweka fedha na kutoa.

Titus alisema pia wanahuduma ya Jumbo ambayo ni akaunti kwa ajili ya watoto.

Alisema akaunti hiyo huwapa watoto fursa ya kuwekezewa fedha zitakazowasaidia katika masomo na maisha yao ya baadae.

Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za Fedha katika Mobile Branch katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Barabara ya Kilwa.
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma za Fedha katika Mobile Branch katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Barabara ya Kilwa.
Gari aina ya Passo ambayo itakabidhiwa kwa mshindi wa mwezi Juni katika viwanja vya Sabasaba.
Ofisa wa Benki ya CRDB, David John akitoa ufafanuzi kuhusu Huduma ya Simbanking kwa mteja aliyefika katika banda la CRDB katika maonyesho ya Sabasaba.
Mteja akipata huduma katika banda la CRDB.
Mteja akiweka sahihi baada ya kufungua akaunti. 
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Pamela Haule akitoa huduma kwa Hawa Hashimu ambaye aliyefika kufungua akaunti katika Viwanja vya Sabasaba.
Ofisa Mauzo wa Benki ya CRDB, Pamela Haule akitoa huduma kwa wateja waliofika katika banda la benki ya CRDB.
Ofisa wa Benki ya CRDB, John Titus (katikati) akimuhudumia mteja wa benki hiyo aliyefika katika banda la benki hiyo, Gerald Stanslaus katika maonyesho ya Sabasaba.
Wateja wakipata huduma katiba banda la CRDB.
Mteja akiweka Passworld baada ya kufungua akaunti. 
Wateja wakipa huduma katika Mobile Branch.

DEGE ECO - VILLAGE WASHIRIKI MAONYESHO YA SABASABA, WATANZANIA WAOMBWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KUNUNUA NYUMBA

Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema “Kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zishakamilika.
Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wa kazi hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika.
 
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village akimhudumia wateja wao aliyefika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village wakiwahudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Muonekano wa Banda lao lililopo viw
 
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village akimhudumia wateja wao waliofika katika banda lao.
Wafanyakazi wa Dege Eco - Village amkimpa maelekezo mteja aliyefika bandani kwao kuchangamkia fursa ya kununua nyumba.
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege Eco-Village (katikati) akiwaonyesha wafanyakazi wa kampuni hiyo namna walivyoweza kufanya vyema katika mauzo ya nyumba.
Wafanyakazi wakiwa katika picha ya pamoja.