Jumanne, 19 Mei 2015

mfanyabiashara maarufu wa madini kizimbani



MFANYABIASHARA maarufu wa Madini ya Tanzanite mkazi wa jijini hapa,Eliakimu Daud Mollel(45),amepandishwa kizimbani katika mahakama
ya hakimu mkazi Arusha akikabiliwa na shitaka la kujipatia madini  ya thamani ya shilingi milioni 15 kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma mashtaka mwishoni mwa wiki, mbele ya hakimu wa mahakama  hiyo,Nestory  Baro,mwendesha mashtaka wa serikali,Gaudencia Lyimo aliieleza mahakama hiyo kwamba, mshtakiwa alitenda kosa hilo januari 4 mwaka huu katika jengo  la Ottu, huku akifahamu  wazi kuwa ni
kinyume cha sheria .

Alisema mshtakiwa huyo alijipatia  madini ya Tanzanite  kutoka kwa mlalamikaji ,Banai Shininu yenye thamani  ya shilingi milioni 15.

Ilidaiwa kuwa mfanyabiashara Mollel alimrubuni mlalamikaji kuwa anaenda kuuza na baadae angemletea kiasi cha shilingi milioni 15,ikiwa ni thamni ya madini hayo, hatua ambayo hakufanya hivyo badala yake alitoweka kusikojulikana.

Mahakama ilielezwa kuwa mshtakiwa alikuwa akitafutwa kwa muda mrefu na mlalamikaji na punde anapopatikana hutoa ahadi za uongo kuwa angelipa kiasi hicho cha fedha lakini hakufanywa hivyo hadi alipokamatwa na kufikishwa mahakamani.

Baada ya kusomewa shtaka hilo la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu,mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo .

Hata hivyo hakimu Baro alimweleza mshtakiwa kwamba  dhamana ipo wazi kwa masharti ya kuwa na fedha tasilimu kiasi cha  shilingi milioni 7.5,na wadhamini wawili wanaofahamika hatua ambayo mshtakiwa alishindwa kutimiza na kulazimika kwenda magereza.

Kesi hiyo namba  88 ya mwaka huu, imepangwa kutajwa tena mahakamani hapo januari 26 mwaka huu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni